24 October 2012

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo woteee!


AIBU HII HADI LINI?




TAARIFA kwamba kontena mbili za pembe za ndovu kutoka Tanzania na Kenya zimekutwa nchini Hong Kong, ni aibu nyingine kwa taifa na ishara kwamba tumeshindwa kudhibiti wizi wa usafirishaji wa nyara za serikali nje ya nchi.

Shehena hiyo ya pembe za ndovu ina thamani ya dola za Marekani milioni 3.4 (wastani wa sh bilioni 5.4).
Pembe hizo, vipande 1,209 vyenye uzito wa tani nne, zilikamatwa juzi nchini humo zikiwa kwenye kontena mbili ambazo ziliwekwa alama kuwa zimebeba plastiki chakavu na maharagwe aina ya roscoco.

Kukamatwa kwa pembe hizo kumekuja wakati serikali ikiwa imeomba upya kwa Umoja wa Mataifa (UN), kuuza akiba yake ya pembe za ndovu zilizotaifishwa ili kupata fedha za kuimarisha ulinzi, kwa lengo la kumaliza tatizo la ujangili.

Tunaandika tahariri hii tukiwa na kumbukumbu ya shehena nyingine ya meno ya tembo iliyokamatwa miaka mitatu iliyopita kwenye makontena kadhaa ughaibuni, na serikali kuahidi kuchukua hatua kali kwa wahusika.

Kashfa kubwa kupita zote iliyowahi kuitingisha nchi na Wizara ya Maliasili na Utalii ni ile ya kusafirisha wanyama hai wapatao 130 nje ya nchi.
Wanyama hao walisafirishwa kwa ndege kubwa ya jeshi la Qatar na taarifa zilidai kuwa walipelekwa katika mji wa Doha nchini humo.


Source: Tanzania Daima; 24/10/2012

No comments:

Post a Comment