15 April 2013

UGUMU WA MAISHA NA ATHARI ZAKE



LEO SAA NNE ASUBUHI WAKATI NASIKILIZA WAPO RADIO STATION, WAKARUSHA HABARI KUWA HUKO KILUVYA KUNA KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 26 LEO ASUBUHI AMEMUA MAMA YAKE KWA KUMPIGA KICHWANI NA KUMTOA UBONGO.

KIJANA HUYO PIA AKASIKIKA AKIKIRI KUWA NI KWELI AMEMUA MAMA YAKEMZAZI  BAADA YA KUONA KUWA MAISHA WANAYOISHI NI MAGUMU SANA, NA MAMA YAKE KUWA AKITESEKA SANA KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA YAO.

MAJIRANI WALIPOHOJIWA KAMA KIJANA HUYO NI MZIMA, WAKASEMA NI MZIMA KABISA WA AKILI INGAWA MARA CHACHE AMEONEKANA AKIWA ANAVUTA BANGI.

KIJANA HUYO AMBAYE HAKUWA AMELALA NYUMBANI JANA USIKU, NA ALIPORUDI LEO ASUBUHI NA KUKUTA WADOGO ZAKE WAMESHAENDA SHULE AKAMUITA MAMA YAKE NA NDIPO ALIPOANZA KUMPIGA KICHWANI KWA NGUVU MARA MBILI NA KUMUUA.




Maisha haya jamani duuuh!









No comments:

Post a Comment