12 August 2013

SAKATA DAWA ZA KULEVYA

MAWAZIRI, wabunge, maaskofu, mapadri, wachungaji wanaohusika uagizaji na uuzaji dawa za kulevya wametakiwa kutubu, kujisalimisha kwa Rais Jakaya Kikwete, vinginevyo majina yao kusambazwa katika balozi zote duniani.


Kauli hiyo ilitolewa  na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga, kutokana na wanafunzi wawili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na St.Gasper cha Morogoro kusalimisha kilo tano za heroine katika kongamano la kidini lililofanyika TAG Mbeya.

Mbali na kujisalimisha vijana hao walitaja mawaziri wawili, Naibu waziri mmoja, wachungaji, baadhi ya wabunge watatu wa viti maalum na wabunge wastaafu wanaomiliki biashara kubwa ndani na nje ya nchi.

Mchungaji Mwamalanga alisema wamesikitishwa na viongozi hao wakuu wa nchi ambao ndio wanatakiwa kuonesha mfano kwa Watanzania kupiga vita dawa za kulevya, lakini wao ndio vinara wakuu wa kuwatumia vijana hao kununua na kuyauza  kinachoshangaza zaidi ni watumishi wa dini, maaskofu, wachungaji nao kuhusika na biashara hii kwa kutumia jina la Mungu kwa namna tofauti na sote tunaonekana tunafanya hivyo,"alisema.


Source: MAJIRA





X-RAY INAYOONYESHA NDANI YA TUMBO LILOBEBA MADAWA YA KULEVYA





Duuuh! Sasa nani msafi jamani? Kwa kweli hii inakatisha tamaa jumlaa!!!

NA WATU WANAYAMUDU VIPI HAYA MADAWA SAFARI NZIMA? SOOO SAD! KWELI TUPIGANE KUDHIBITI TATIZO HILI KUBWA! UBINADAMU UMEKWISHA JUMLA!!!


No comments:

Post a Comment