14 August 2012

MJI WA WANAWAKE TU! - SAUDI ARABIA



Nchini Saudi Arabia tayari kuna vyuo vikuu, Ofisi na hata migahawa inavyowatenganisha watu kutokana na jinsia zao.
Kwa sasa tayari mji mmoja wa viwanda unaonuiwa kuwa wa wanawake pekee ujulikanao kama Hofuf umeanza kustawishwa Mashariki mwa taifa hilo.
Serikali imeahidi kuwa miji mingine ya wanawake pekee itajengwa katika maeneo mengine ya nchi.
Juhudi hizo ni mojawapo ya mipango ya Serikali ya kutoa nafasi nyingi zaidi za kazi kwa wanawake ambao wanashikilia asilimia 15 pekee ya wafanyakazi nchini, ingawa wanawake wengi zaidi ndio wanaofuzu na vyeti vya shahada ya kwanza katika vyuo vikuu kuwazidi wanaume.
Mkereketwa wa haki za wanawake nchini Saudi Arabia, Reem Asaad, anasema kwamba wanawake wanapendelea zaidi kufanya kazi wakiwa mbali na wanaume.
Alisema mwamko huu mpya ni sehemu moja ya mpango maalumu wa kuwapa uhuru wa kifedha zaidi wanawake katika himaya hiyo.

No comments:

Post a Comment