20 January 2014

BABA PANYA NA MKIA WA MWANAE










Jinsi siasa za ki-CCM zilivyo ni rahisi tukalinganisha na yanayotokea serikalini na kisa hiki:

Panya wamejitahidi sana kumkwepa paka kwa kukimbilia shimoni kila wanapoona na kuhisi harufu ya paka karibu yao. Leo, mambo yamebadilika. Paka katokea ghafla. Kufumba na kufumbua panya wote wamekimbilia shimoni. Bahati mbaya mtoto wa panya ameingia shimoni wa mwisho na kausahau mkia wake nje. Paka kauona mkia katika mdomo wa shimo. Katoa sauti ya mguno huku akisema naona mkia hapa. Panya wote shimoni wamemsikia paka huko nje. Panya wamegundua hatari inawasubiria huko nje.

Baba panya kafura kwa hasira, anafoka, " Nani mwenye mkia humu!? Panya wote mabibi na mabwana wamenyamaza kimya. Baba panya anapoinuka kwenye kiti ili ambaini mwenye mkia. Anabaini naye anao mkia; tena wa kwake ni mkubwa harafu mrefu. Kuona hivyo, baba panya anarejea kuketi kitini pake kimya kimya!

Lo! Wote kumbe wana mikia!!!

CCM hakika ni chama cha mizigo, magamba, mafisadi, wala rushwa, wang'oa kucha, warusha mabomu makanisani na mikutanoni. Je! Wewe umeona wamwaga tindikali wakikamatwa?....au umeona warusha mabomu wakikamatwa?....au watekaji na wang'oa kucha bila ganzi wakikamatwa?



SOURCE: JAMII FORUM



Mie sio mpenzi wa SIASA kabisaaa! Ndio maana huwa si post siasa kwenye blog yangu. But hii story imenichekesha sana sana leo!!!

1 comment:

  1. Shosti unawachokozaaa..aahh kumbe source siyo wewe..basi wakuache tu shosti wangu wee unafikisha ujumbe tu...ila duuh hii story si mchezo.

    ReplyDelete