14 August 2013

DR. MWAKYEMBE NA MADAWA YA KULEVYA




Mwakyembe avunja ukimya, asema "siku 14 zinatosha kuwanasa wasafirishaji wa dawa za kulevya"


Amesema sasa watakiona cha moto, atawakamata ndani ya wiki mbili.
"Nitahakikisha nawabana watumishi wa Uwanja wa Ndege waeleze jinsi dawa zinavyopitishwa katika uwanja huo na wahusika ni akina nani.



From Jamii Forum; (Chanzo: Majira, Jumatano )




DR. MWAKYEMBE ATAFUTA MCHAWI


HATMA ya maofisa wanaoruhusu kupitishwa dawa za kulevya katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), imewadia kufuatia Waziri wa Uchukuzi, Dk 
Harrison Mwakyembe, kuwaweka kitimoto viongozi wa idara nne watoe taarifa ni kwa nini uwanja huo umekuwa uchochoro wa kupitisha dawa hizo.


Pia ametaka maofisa hao kutoka idara ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kutaja majina ya watumishi wanaohusika kula njama na wasafirishaji wa dawa za kulevya kupitia uwanja huo ili aweze kuwachukulia hatua.


"Bado naendelea na vikao, kifupi nimetaka maofisa wa TAA, Anga, Polisi na Usalama wa Taifa wanipe taarifa haraka ni kwa nini uwanja wa JNIA umekuwa uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya", alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza "nataka wataje wahusika wa biashara ya dawa za kulevya, nani aliacha mwanya hadi watu hao wakapita na dawa hizo, baada ya hapo ntachukua hatua",
Kabla ya kuwaweka kitimoto maofisa wa idara hizo, Dr Mwakyembe alifika katika uwanja wa JNIA kuzindua Kamati mpya ya Taifa ya Usalama wa Anga.





Source: NIPASHE; 8th, August, 13 






ALL THE BEST MR. MWAKYEMBE, TUKO NYUMA YAKO ALL THE WAY NA MUNGU AKULINDE KWENYE MAPAMBANO HAYA MAKUBWA!!!

No comments:

Post a Comment