21 August 2013

IT'S TIME WE MOVE ON FROM ALL THESE MANENO



Dar es Salaam. Uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda unazidi kudorora kutokana vyombo vya habari na baadhi ya maofisa wa nchi hiyo kuanza ‘kuichokonoa familia ya Rais Jakaya Kikwete’.
Tovuti ya News of Rwanda, imedai kuwa mke wa Rais, Salma Kikwete ni ndugu wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana ambaye aliuawa kwenye ajali ya ndege wakati akitokea nchini Tanzania mwaka 1993.
Madai hayo yametokana na mtandao wa Wiki Leaks, ambao ulinasa mawasiliano kati ya Ubalozi wa Marekani nchini na Serikali ya nchi hiyo. Kadhalika taarifa hiyo ya Wiki Leaks imenukuliwa na magazeti mengine ya Rwanda likiwamo gazeti maarufu la New Times.
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amekanusha taarifa hizo zinazodai kuwa Rais Kikwete ni shemeji yake na Habyarimana.



Source: Mwananchi



No comments:

Post a Comment