29 August 2013

GOOO M-SOKA

20130817_132318

Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni Afrisoft Technologies Ltd Brian Mushi, Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni hiyo David Kagoma pamoja na Msimamizi wa Fedha Bw. Bujune Leo kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-soka.

Kampuni ya Afrisoft Technologies Ltd inayojihusisha na masuala ya teknolojia zinazorahisisha maisha ya kila siku, sasa imekuja na huduma mpya ya ‘M-Soka’ ambapo mtumiaji wa mtandao wa Vodacom anaweza kufaidi huduma hiyo kwa muda wowote na kwa haraka zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Brian Godwin Mushi amesema wameamua kutengeneza huduma hiyo, kwa kuwa mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi na hivyo ukizingatia mahitaji ya watu kutaka kujua matokeo au kujua ratiba, sasa haina haja tena kusubiri gazeti au redio ila ukiingia katika ‘M-Soka’ (Mobile Soka)unapata kila kitu moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.
Bw. Mushi amesema ukizingatia hali halisi sio kila mahali panapatikana huduma ya intaneti na sio kila mtu ana simu inayoweza kuunganishwa kwenye mtandao huo, hivyo kupitia ‘M-Soka’ unaweza kupata 
matokeo au ratiba kwa kutumia simu ya aina yeyote ile.
Akitaja namba zinazotumika kupata matokeo hayo amesema kuwa ni *149*31# kwa gharama nafuu ya shilingi 40 tu.








HONGERA BRIAN!!!! SOOOO PROUD OF YOU BABY BROTHER!!! GOD BLESS!

No comments:

Post a Comment