26 June 2012

USAGAJI UNAVYOSHAMIRI SOKA YA WANAWAKE


VITENDO vya usagaji vimekuwa vikitajwa mara kwa mara hasa kwenye timu za soka za wanawake kutokana na mazingira ya mikusanyiko ya wasichana wenye hulka mbalimbali wanaokaa pamoja.

Vitendo hivyo ni pale wasichana ama wanawake wanapokuwa wanastareheshana. 

Katikati ya wiki iliyopita, aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya soka Wanawake (Twiga Stars), Boniface Mkwasa alitangaza kubwaga manyanga huku akiacha 'kibomu' kuwa baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars ni wasagaji.

Mkwasa alisema kuwa walitumia njia mbalimbali na kuwaengua kutoka miongoni mwa wachezaji wake huku akisema alikuwa akikerwa na baadhi ya wachezaji waliokuwa na tabia hiyo.
Nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alitoa kauli hiyo wakati alipopata fursa kueleza sababu za kujiuzulu kufundisha Twiga Stars.

Kiungo huyo wa zamani ndiye aliyeiwezesha Twiga kuandika historia kwa kucheza mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake mwaka jana nchini Afrika Kusini.

SOURCE: MWANANCHI, 25/06/12

No comments:

Post a Comment