29 October 2012

AMANI AMANI

WAIMBAJI nchini, wametakiwa kujipanga na kutumia nafasi yao ili kuhakikisha wanaihamasisha jamii kwa njia ya uimbaji ili amani iliyopo iendelee kudumishwa.

Akizungumza mara baada ya kutoka katika ibada iliyofanyika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God la jijini Dar es Salaam, malkia wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando, alisema kuwa waimbaji wana uwezo wa kuishawishi jamii ikaweza kubadilika.

Muhando alisema kuwa kutokana na vurugu zinazojitokeza nchini, kuna umuhimu wa waimbaji kuhakikisha wanatunga nyimbo zitakazohamasisha kulinda amani ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa.


Source: Tanzania Daima


"IF SOMEONE THINKS THAT PEACE AND LOVE ARE JUST A CLICHE THAT MUST HAVE BEEN LEFT  BEHIND IN 1960'S, THAT'S A PROBLEM. LOVE AND PEACE  ARE ETERNAL." JOHN LENNON

No comments:

Post a Comment