24 October 2012

Waziri afanya mambo




Hapa alipokuwa na Hasheem Thabeet katika launching ya basketball clinic in Dar




NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amemwaibisha Rais Jakaya Kikwete na taifa kwa ujumla mbele ya jamii ya kimataifa, baada ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania imetokana na muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na Tanganyika.
Mbali na hilo, aliwaambia mamia ya wajumbe kutoka mataifa mbalimbali katika Bara la Afrika kuwa, Tanzania ilizaliwa mwaka 11964.

“Wasilisho langu litakuwa na sehemu saba…Utangulizi, Tanzania iliundwa mwaka 11964 kwa kuunganisha visiwa vya Bahari ya Hindi vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na nchi ya Bara iliyokuwa ikiitwa Tanganyika…,” alisema Naibu Waziri Mulugo kwa kujiamini na bila kuonyesha dalili yoyote kuwa alikuwa amekosea.
Naibu waziri huyo alikuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa viongozi na wataalamu wa elimu katika Bara la Afrika, ambao ulifanyika Afrika Kusini kuanzia Oktoba 5-7, mwaka huu.

Kuboronga huko kwa naibu waziri huyo kumeibua mjadala mkubwa na mzito miongoni mwa Watanzania wa kada na rika mbalimbali, huku wengi wakianza kupata wasiwasi juu ya uwezo wa watu wanaoteuliwa na Rais Kikwete kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

Na George Maziku



Source: Tanzania Daima; 24/10/12

No comments:

Post a Comment