27 October 2012


Hatimaye usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam, utaanza rasmi keshokutwa, Jumatatu baada ya maandalizi yote kukamilika.
Kuanza kwa usafiri huo, ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, katika kikao cha Bunge cha bajeti ambapo alisema usafiri huo ungeanza Oktoba mwaka huu.
Treni zitakuwa kazini kuanzia saa 5.00 asubuhi hadi saa tatu usiku. Nauli zitakuwa sh.100 kwa watoto na wanafunzi na 400 kwa watu wazima kwa treni ya kuanzia katikati ya mji mpaka ubungo maziwa. Kwa treni ya Tazara itakayoanzia Dar es Salaam kwenda Mwakanga nauli itakuwa sh. 500 kwa mtu mzima, na watoto sh.100

Source: Mwananchi 27/10/12


No comments:

Post a Comment